Psalms 39
1Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu 2 na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; 1 nitaweka lijamu kinywani mwangu 2 wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” 1
2Lakini niliponyamaza kimya na kutulia, 2 hata pasipo kusema lolote jema, 2 uchungu wangu uliongezeka. 1
3Moyo wangu ulipata moto ndani yangu, 2 nilipotafakari, moto uliwaka, 2 ndipo nikasema kwa ulimi wangu: 1
4“Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu 2 na hesabu ya siku zangu; 1 nijalie kujua jinsi maisha yangu 2 yanavyopita upesi. 1
5Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; 2 muda wangu wa kuishi ni kama 2 hauna thamani kwako. 1 Maisha ya kila mwanadamu 2 ni kama pumzi. 1
6Hakika kila binadamu ni kama njozi 2 aendapo huku na huko: 1 hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; 2 anakusanya mali nyingi, 2 wala hajui ni nani atakayeifaidi. 1
7“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? 2 Tumaini langu ni kwako. 1
8Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, 2 usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu. 1
9Nilinyamaza kimya, 2 sikufumbua kinywa changu, 2 kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili. 1
10Niondolee mjeledi wako, 2 nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako. 1
11Unakemea na kuadhibu wanadamu 2 kwa ajili ya dhambi zao; 1 unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: 2 kila mwanadamu ni kama pumzi tu. 1
12“Ee Bwana, usikie maombi yangu, 2 usikie kilio changu unisaidie, 2 usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. 1 Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, 2 kama walivyokuwa baba zangu wote, 1
13Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena 2 kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”