Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 135

1Msifuni Bwana. 1 Lisifuni jina la Bwana, 2 msifuni, enyi watumishi wa Bwana, 1

2ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, 2 katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. 1

3Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, 2 liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. 1

4Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, 2 Israeli kuwa mali yake ya thamani. 1

5Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, 2 kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote. 1

6Bwana hufanya lolote apendalo, 2 mbinguni na duniani, 2 katika bahari na vilindi vyake vyote. 1

7Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; 2 hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua 2 na huleta upepo kutoka ghala zake. 1

8Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, 2 mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama. 1

9Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, 2 dhidi ya Farao na watumishi wake wote. 1

10Aliyapiga mataifa mengi, 2 na akaua wafalme wenye nguvu: 1

11Mfalme Sihoni na Waamori, 2 Ogu mfalme wa Bashani 2 na wafalme wote wa Kanaani: 1

12akatoa nchi yao kuwa urithi, 2 urithi kwa watu wake Israeli. 1

13Ee Bwana, jina lako ladumu milele, 2 kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote. 1

14Maana Bwana atawathibitisha watu wake, 2 na kuwahurumia watumishi wake. 1

15Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, 2 zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 1

16Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, 2 zina macho, lakini haziwezi kuona; 1

17zina masikio, lakini haziwezi kusikia, 2 wala hakuna pumzi katika vinywa vyao. 1

18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, 2 vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. 1

19Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; 2 ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana; 1

20ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; 2 ninyi mnaomcha, msifuni Bwana. 1

21Msifuni Bwana kutoka Sayuni, 2 msifuni yeye aishiye Yerusalemu. 1 Msifuni Bwana.

← Psalms 134Read In The App, Free →Psalms 136 →

Study Psalms 135

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150