Psalms 4
1Nijibu nikuitapo, 2 Ee Mungu wangu mwenye haki! 1 Nipumzishe katika shida zangu; 2 nirehemu, usikie ombi langu. 1
2Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu 2 kuwa aibu mpaka lini? 1 Mtapenda udanganyifu 2 na kufuata miungu ya uongo mpaka lini? 1
3Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga 2 wale wamchao kwa ajili yake; 2 Bwana atanisikia nimwitapo. 1
4Katika hasira yako, usitende dhambi. 2 Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya 2 mkiichunguza mioyo yenu. 1
5Toeni dhabihu zilizo haki; 2 mtegemeeni Bwana. 1
6Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye 2 kutuonyesha jema lolote?” 2 Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako. 1
7Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa 2 kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi. 1
8Nitajilaza chini na kulala kwa amani, 2 kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana, 2 waniwezesha kukaa kwa salama.