Psalms 119
1Heri wale walio waadilifu katika njia zao, 2 wanaoenenda katika sheria ya Bwana. 1
2Heri wale wanaozishika shuhuda zake, 2 wamtafutao kwa moyo wao wote. 1
3Wasiofanya lolote lililo baya, 2 wanaoenenda katika njia zake. 1
4Umetoa maagizo yako 2 ili tuyatii kwa ukamilifu. 1
5Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara 2 katika kuyatii maagizo yako! 1
6Hivyo mimi sitaaibishwa 2 ninapozingatia amri zako zote. 1
7Nitakusifu kwa moyo mnyofu 2 ninapojifunza sheria zako za haki. 1
8Nitayatii maagizo yako; 2 usiniache kabisa. 2 Kutii Sheria Ya Bwana 1
9Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? 2 Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. 1
10Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, 2 usiniache niende mbali na amri zako. 1
11Nimelificha neno lako moyoni mwangu 2 ili nisikutende dhambi. 1
12Sifa ni zako, Ee Bwana, 2 nifundishe maagizo yako. 1
13Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote 2 zinazotoka katika kinywa chako. 1
14Ninafurahia kufuata sheria zako 2 kama mtu afurahiaye mali nyingi. 1
15Ninatafakari maagizo yako 2 na kuziangalia njia zako. 1
16Ninafurahia maagizo yako, 2 wala sitalipuuza neno lako. 2 Furaha Katika Sheria Ya Bwana 1
17Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; 2 nitalitii neno lako. 1
18Yafungue macho yangu nipate kuona 2 mambo ya ajabu katika sheria yako. 1
19Mimi ni mgeni duniani, 2 usinifiche amri zako. 1
20Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa 2 juu ya sheria zako wakati wote. 1
21Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa 2 waendao mbali na amri zako. 1
22Niondolee dharau na dhihaka, 2 kwa kuwa ninazishika sheria zako. 1
23Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, 2 mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako. 1
24Sheria zako ni furaha yangu, 2 nazo ni washauri wangu. 2 Kuamua Kuitii Sheria Ya Bwana 1
25Nimelazwa chini mavumbini, 2 yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. 1
26Nilikueleza njia zangu ukanijibu, 2 nifundishe sheria zako. 1
27Nijulishe mafundisho ya mausia yako, 2 nami nitatafakari maajabu yako. 1
28Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, 2 uniimarishe sawasawa na neno lako. 1
29Niepushe na njia za udanganyifu, 2 kwa neema unifundishe sheria zako. 1
30Nimechagua njia ya kweli, 2 nimekaza moyo wangu katika sheria zako. 1
31Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, 2 usiniache niaibishwe. 1
32Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, 2 kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru. 2 Maombi Ili Kupata Ufahamu Wa Sheria 1
33Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, 2 nami nitayashika mpaka mwisho. 1
34Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako 2 na kuitii kwa moyo wangu wote. 1
35Niongoze kwenye njia ya amri zako, 2 kwa kuwa huko napata furaha. 1
36Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, 2 na siyo kwenye mambo ya ubinafsi. 1
37Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, 2 uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. 1
38Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, 2 ili upate kuogopwa. 1
39Niondolee aibu ninayoiogopa, 2 kwa kuwa sheria zako ni njema. 1
40Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! 2 Hifadhi maisha yangu katika haki yako. 2 Kuitumainia Sheria Ya Bwana 1
41Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, 2 wokovu wako sawasawa na ahadi yako, 1
42ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, 2 kwa kuwa ninalitumainia neno lako. 1
43Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, 2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako. 1
44Nitaitii amri yako daima, 2 naam, milele na milele. 1
45Nitatembea nikiwa huru, 2 kwa kuwa nimejifunza mausia yako. 1
46Nitasema sheria zako mbele za wafalme 2 wala sitaaibishwa, 1
47kwa kuwa ninazifurahia amri zako 2 kwa sababu ninazipenda. 1
48Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, 2 nami ninatafakari juu ya maagizo yako. 2 Matumaini Katika Sheria Ya Bwana 1
49Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, 2 kwa sababu umenipa tumaini. 1
50Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: 2 Ahadi yako inahifadhi maisha yangu. 1
51Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, 2 hata hivyo sitaiacha sheria yako. 1
52Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, 2 nazo zinanifariji. 1
53Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, 2 ambao wameacha sheria yako. 1
54Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu 2 popote ninapoishi. 1
55Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, 2 nami nitatii sheria yako. 1
56Hili limekuwa zoezi langu: 2 nami ninayatii mausia yako. 2 Kujitolea Katika Sheria Ya Bwana 1
57Ee Bwana, wewe ni fungu langu, 2 nimeahidi kuyatii maneno yako. 1
58Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, 2 nihurumie sawasawa na ahadi yako. 1
59Nimezifikiri njia zangu 2 na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako. 1
60Nitafanya haraka bila kuchelewa 2 kuzitii amri zako. 1
61Hata waovu wanifunge kwa kamba, 2 sitasahau sheria yako. 1
62Usiku wa manane ninaamka kukushukuru 2 kwa sababu ya sheria zako za haki. 1
63Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao, 2 kwa wote wanaofuata mausia yako. 1
64Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, 2 nifundishe maagizo yako. 2 Thamani Ya Sheria Ya Bwana 1
65Mtendee wema mtumishi wako 2 Ee Bwana, sawasawa na neno lako. 1
66Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, 2 kwa kuwa ninaamini amri zako. 1
67Kabla sijapata shida nilipotea njia, 2 lakini sasa ninalitii neno lako. 1
68Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, 2 nifundishe maagizo yako. 1
69Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, 2 nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote. 1
70Mioyo yao ni katili na migumu, 2 bali mimi napendezwa na sheria yako. 1
71Ilikuwa vyema mimi kupata shida 2 ili nipate kujifunza maagizo yako. 1
72Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu 2 kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu. 2 Haki Ya Sheria Ya Bwana 1
73Mikono yako ilinifanya na kuniumba, 2 nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako. 1
74Wakuchao wafurahie wanaponiona, 2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako. 1
75Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, 2 katika uaminifu wako umeniadhibu. 1
76Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, 2 sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. 1
77Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, 2 kwa kuwa naifurahia sheria yako. 1
78Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, 2 lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako. 1
79Wale wakuchao na wanigeukie mimi, 2 hao ambao wanazielewa sheria zako. 1
80Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, 2 ili nisiaibishwe. 2 Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa 1
81Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, 2 lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako. 1
82Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; 2 ninasema, “Utanifajiri lini?” 1
83Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, 2 bado sijasahau maagizo yako. 1
84Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? 2 Ni lini utawaadhibu washtaki wangu? 1
85Wenye majivuno wananichimbia mashimo, 2 kinyume na sheria yako. 1
86Amri zako zote ni za kuaminika; 2 unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu. 1
87Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, 2 lakini sijaacha mausia yako. 1
88Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, 2 nami nitatii sheria za kinywa chako. 2 Imani Katika Sheria Ya Bwana 1
89Ee Bwana, neno lako ni la milele, 2 linasimama imara mbinguni. 1
90Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, 2 umeiumba dunia, nayo inadumu. 1
91Sheria zako zinadumu hadi leo, 2 kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia. 1
92Kama nisingefurahia sheria yako, 2 ningeangamia katika taabu zangu. 1
93Sitasahau mausia yako kamwe, 2 kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu. 1
94Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, 2 kwa kuwa nimetafuta mausia yako. 1
95Waovu wanangojea kuniangamiza, 2 bali mimi ninatafakari sheria zako. 1
96Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, 2 lakini amri zako hazina mpaka. 2 Kuipenda Sheria Ya Bwana 1
97Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. 2 Ninaitafakari mchana kutwa. 1
98Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, 2 kwa kuwa nimezishika daima. 1
99Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, 2 kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako. 1
100Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, 2 kwa kuwa ninayatii mausia yako. 1
101Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, 2 ili niweze kutii neno lako. 1
102Sijaziacha sheria zako, 2 kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. 1
103Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, 2 matamu kuliko asali katika kinywa changu! 1
104Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, 2 kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu. 2 Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana 1
105Neno lako ni taa ya miguu yangu 2 na mwanga katika njia yangu. 1
106Nimeapa na nimethibitisha, 2 kwamba nitafuata sheria zako za haki. 1
107Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, 2 sawasawa na neno lako. 1
108Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, 2 nifundishe sheria zako. 1
109Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, 2 sitasahau sheria yako. 1
110Waovu wamenitegea mtego, 2 lakini sijayakiuka maagizo yako. 1
111Sheria zako ni urithi wangu milele, 2 naam ni furaha ya moyo wangu. 1
112Nimekusudia moyoni mwangu 2 kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho. 2 Usalama Ndani Ya Sheria Ya Bwana 1
113Ninachukia watu wa nia mbili, 2 lakini ninapenda sheria yako. 1
114Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, 2 nimeweka tumaini langu katika neno lako. 1
115Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, 2 ili niweze kushika amri za Mungu wangu! 1
116Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; 2 usiache matumaini yangu yakavunjwa. 1
117Nitegemeze, nami nitaokolewa, 2 nami daima nitayaheshimu maagizo yako. 1
118Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, 2 kwa maana udanganyifu wao ni bure. 1
119Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, 2 kwa hivyo nazipenda sheria zako. 1
120Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, 2 ninaziogopa sheria zako. 2 Kuitii Sheria Ya Bwana 1
121Nimetenda yaliyo haki na sawa, 2 usiniache mikononi mwa watesi wangu. 1
122Mhakikishie mtumishi wako usalama, 2 usiache wenye kiburi wanionee. 1
123Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, 2 na kuitazamia ahadi yako ya kweli. 1
124Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako 2 na unifundishe maagizo yako. 1
125Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu 2 ili niweze kuelewa sheria zako. 1
126Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, 2 kwa kuwa sheria yako inavunjwa. 1
127Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, 2 naam, zaidi ya dhahabu safi, 1
128na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, 2 nachukia kila njia potovu. 2 Shauku Ya Kuitii Sheria Ya Bwana 1
129Sheria zako ni za ajabu, 2 hivyo ninazitii. 1
130Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, 2 kunampa mjinga ufahamu. 1
131Nimefungua kinywa changu na kuhema, 2 nikitamani amri zako. 1
132Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote 2 wale wanaolipenda jina lako. 1
133Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, 2 usiache dhambi yoyote initawale. 1
134Niokoe na uonevu wa wanadamu, 2 ili niweze kutii mausia yako. 1
135Mwangazie mtumishi wako uso wako 2 na unifundishe amri zako. 1
136Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, 2 kwa kuwa sheria yako haifuatwi. 2 Haki Ya Sheria Ya Bwana 1
137Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, 2 sheria zako ni sahihi. 1
138Sheria ulizoziweka ni za haki, 2 ni za kuaminika kikamilifu. 1
139Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu 2 wanayapuuza maneno yako. 1
140Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, 2 mtumishi wako anazipenda. 1
141Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, 2 sisahau mausia yako. 1
142Haki yako ni ya milele, 2 na sheria yako ni kweli. 1
143Shida na dhiki zimenipata, 2 lakini amri zako ni furaha yangu. 1
144Sheria zako ni sahihi milele, 2 hunipa ufahamu ili nipate kuishi. 2 Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa 1
145Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote, 2 nami nitayatii maagizo yako. 1
146Ninakuita; niokoe 2 nami nitazishika sheria zako. 1
147Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; 2 nimeweka tumaini langu katika neno lako. 1
148Sikufumba macho yangu usiku kucha, 2 ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. 1
149Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, 2 Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako. 1
150Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, 2 lakini wako mbali na sheria yako. 1
151Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu, 2 na amri zako zote ni za kweli. 1
152Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako 2 kwamba umezithibitisha ili zidumu milele. 2 Maombi Kwa Ajili Ya Msaada 1
153Yaangalie mateso yangu, uniokoe, 2 kwa kuwa sijasahau sheria yako. 1
154Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, 2 uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako. 1
155Wokovu uko mbali na waovu, 2 kwa kuwa hawatafuti maagizo yako. 1
156Ee Bwana, huruma zako ni kuu, 2 uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako. 1
157Adui wanaonitesa ni wengi, 2 lakini mimi sitaziacha sheria zako. 1
158Ninawatazama wasioamini kwa chuki, 2 kwa kuwa hawalitii neno lako. 1
159Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; 2 Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako. 1
160Maneno yako yote ni kweli, 2 sheria zako zote za haki ni za milele. 2 Kujiweka Wakfu Kwa Sheria Ya Bwana 1
161Watawala wamenitesa bila sababu, 2 lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako. 1
162Nafurahia ahadi zako 2 kama mtu aliyepata mateka mengi. 1
163Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, 2 lakini napenda sheria yako. 1
164Ninakusifu mara saba kwa siku, 2 kwa ajili ya sheria zako za haki. 1
165Wanaopenda sheria yako wana amani tele, 2 wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza. 1
166Ee Bwana, ninangojea wokovu wako, 2 nami ninafuata amri zako, 1
167Ninazitii sheria zako, 2 kwa sababu ninazipenda mno. 1
168Nimetii mausia yako na sheria zako, 2 kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako. 2 Kuomba Msaada 1
169Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako, 2 nipe ufahamu sawasawa na neno lako. 1
170Maombi yangu na yafike mbele zako, 2 niokoe sawasawa na ahadi yako. 1
171Midomo yangu na ibubujike sifa, 2 kwa kuwa unanifundisha maagizo yako. 1
172Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, 2 kwa kuwa amri zako zote ni za haki. 1
173Mkono wako uwe tayari kunisaidia, 2 kwa kuwa nimechagua mausia yako. 1
174Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, 2 na sheria yako ni furaha yangu. 1
175Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, 2 na sheria zako zinitegemeze. 1
176Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. 2 Mtafute mtumishi wako, 2 kwa kuwa sijasahau amri zako.