Psalms 65
1Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; 2 kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. 1
2Ewe usikiaye maombi, 2 kwako wewe watu wote watakuja. 1
3Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, 2 wewe ulisamehe makosa yetu. 1
4Heri wale uliowachagua 2 na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! 1 Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, 2 mema ya Hekalu lako takatifu. 1
5Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, 2 Ee Mungu Mwokozi wetu, 1 tumaini la miisho yote ya duniani 2 na la bahari zilizo mbali sana, 1
6uliyeumba milima kwa uwezo wako, 2 ukiwa umejivika nguvu, 1
7uliyenyamazisha dhoruba za bahari, 2 ngurumo za mawimbi yake, 2 na ghasia za mataifa. 1
8Wale wanaoishi mbali sana 2 wanaogopa maajabu yako, 1 kule asubuhi ipambazukiapo 2 na kule jioni inakofifilia 2 umeziita nyimbo za furaha. 1
9Waitunza nchi na kuinyeshea, 2 waitajirisha kwa wingi. 1 Vijito vya Mungu vimejaa maji 2 ili kuwapa watu nafaka, 2 kwa maana wewe umeviamuru. 1
10Umeilowesha mifereji yake 2 na kusawazisha kingo zake; 1 umeilainisha kwa manyunyu 2 na kuibariki mimea yake. 1
11Umeuvika mwaka taji ya baraka, 2 magari yako yanafurika kwa wingi. 1
12Mbuga za majani za jangwani umezineemesha; 2 vilima vimevikwa furaha. 1
13Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama, 2 na mabonde yamepambwa kwa mavuno; 2 vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.