Psalms 138
1Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote, 2 mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. 1
2Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, 2 nami nitalisifu jina lako 1 kwa ajili ya upendo wako 2 na uaminifu, 1 kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako 2 juu ya vitu vyote. 1
3Nilipoita, ulinijibu; 2 ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. 1
4Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana, 2 wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. 1
5Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana, 2 kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu. 1
6Ingawa Bwana yuko juu, 2 humwangalia mnyonge, 1 bali mwenye kiburi 2 yeye anamjua kutokea mbali. 1
7Nijapopita katikati ya shida, 2 wewe unayahifadhi maisha yangu, 1 unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, 2 kwa mkono wako wa kuume unaniokoa. 1
8Bwana atatimiza kusudi lake kwangu, 2 Ee Bwana, upendo wako wadumu milele: 2 usiziache kazi za mikono yako.