Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 97

1Bwana anatawala, nchi na ifurahi, 2 visiwa vyote vishangilie. 1

2Mawingu na giza nene vinamzunguka, 2 haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi. 1

3Moto hutangulia mbele zake 2 na huteketeza adui zake pande zote. 1

4Umeme wake wa radi humulika dunia, 2 nchi huona na kutetemeka. 1

5Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana, 2 mbele za Bwana wa dunia yote. 1

6Mbingu zinatangaza haki yake, 2 na mataifa yote huona utukufu wake. 1

7Wote waabuduo sanamu waaibishwa, 2 wale wajisifiao sanamu: 2 mwabuduni yeye, enyi miungu yote! 1

8Sayuni husikia na kushangilia, 2 vijiji vya Yuda vinafurahi 2 kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana. 1

9Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; 2 umetukuka sana juu ya miungu yote. 1

10Wale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu, 2 kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake 2 na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu. 1

11Nuru huangaza wenye haki 2 na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. 1

12Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki, 2 lisifuni jina lake takatifu.

← Psalms 96Read In The App, Free →Psalms 98 →

Study Psalms 97

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150