Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 59

1Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, 2 unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. 1

2Uniponye na watu watendao mabaya, 2 uniokoe kutokana na wamwagao damu. 1

3Tazama wanavyonivizia! 2 Watu wakali wananifanyia hila, 1 ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea 2 wala kutenda dhambi. 1

4Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. 2 Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya! 1

5Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! 2 Zinduka uyaadhibu mataifa yote, 2 usionyeshe huruma kwa wasaliti. 1

6Hurudi wakati wa jioni, 2 wakibweka kama mbwa, 2 wakiuzurura mji. 1

7Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, 2 hutema upanga kutoka midomo yao, 2 nao husema, “Ni nani atakayetusikia?” 1

8Lakini wewe, Bwana, uwacheke; 2 unayadharau mataifa hayo yote. 1

9Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, 2 wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, 2

10Mungu wangu unipendaye. 1 Mungu atanitangulia, 2 naye atanifanya niwachekelee 2 wale wanaonisingizia. 1

11Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, 2 au sivyo watu wangu watasahau. 1 Katika uwezo wako wafanye watangetange 2 na uwashushe chini. 1

12Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, 2 kwa ajili ya maneno ya midomo yao, 2 waache wanaswe katika kiburi chao. 1 Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, 2

13wateketeze katika ghadhabu, 2 wateketeze hadi wasiwepo tena. 1 Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia 2 kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo. 1

14Hurudi jioni, 2 wakibweka kama mbwa, 2 wakiuzurura mji. 1

15Wanatangatanga wakitafuta chakula, 2 wasipotosheka hubweka kama mbwa. 1

16Lakini mimi nitaziimba nguvu zako, 2 asubuhi nitaimba juu ya upendo wako; 1 kwa maana wewe ndiwe ngome yangu 2 na kimbilio langu wakati wa shida. 1

17Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa. 2 Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, 2 Mungu unipendaye.

← Psalms 58Read In The App, Free →Psalms 60 →

Study Psalms 59

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150