Psalms 75
1Ee Mungu, tunakushukuru, 2 tunakushukuru wewe, 1 kwa kuwa jina lako li karibu; 2 watu husimulia matendo yako ya ajabu. 1
2Unasema, “Ninachagua wakati maalum; 2 ni mimi nihukumuye kwa haki. 1
3Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, 2 ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara. 1
4Kwa wale wenye majivuno ninasema, 2 ‘Msijisifu tena,’ 2 kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu. 1
5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; 2 msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ” 1
6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi 2 au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. 1
7Bali Mungu ndiye ahukumuye: 2 Humshusha huyu na kumkweza mwingine. 1
8Mkononi mwa Bwana kuna kikombe 2 kilichojaa mvinyo unaotoka povu 2 uliochanganywa na vikolezo; 1 huumimina, nao waovu wote wa dunia 2 hunywa mpaka tone la mwisho. 1
9Bali mimi, nitatangaza hili milele; 2 nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. 1
10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, 2 bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.