Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 72

1Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, 2 mwana wa mfalme kwa haki yako. 1

2Atawaamua watu wako kwa haki, 2 watu wako walioonewa kwa haki. 1

3Milima italeta mafanikio kwa watu, 2 vilima tunda la haki. 1

4Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu 2 na atawaokoa watoto wa wahitaji, 2 ataponda mdhalimu. 1

5Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote. 1

6Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, 2 kama manyunyu yanyeshayo ardhi. 1

7Katika siku zake wenye haki watastawi; 2 mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma. 1

8Atatawala kutoka bahari hadi bahari 2 na kutoka Mto + 72:8 Yaani Mto Frati. mpaka miisho ya dunia. 1

9Makabila ya jangwani watamsujudia, 2 na adui zake wataramba mavumbi. 1

10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali 2 watamletea kodi; 1 wafalme wa Sheba na Seba 2 watampa zawadi. 1

11Wafalme wote watamsujudia 2 na mataifa yote yatamtumikia. 1

12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, 2 aliyeonewa asiye na wa kumsaidia. 1

13Atawahurumia wanyonge na wahitaji 2 na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. 1

14Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, 2 kwani damu yao ni ya thamani machoni pake. 1

15Aishi maisha marefu! 2 Na apewe dhahabu ya Sheba. 1 Watu wamwombee daima 2 na kumbariki mchana kutwa. 1

16Nafaka ijae tele katika nchi yote, 2 juu ya vilele vya vilima na istawi. 1 Tunda lake na listawi kama Lebanoni, 2 listawi kama majani ya kondeni. 1

17Jina lake na lidumu milele, 2 na lidumu kama jua. 1 Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, 2 nao watamwita aliyebarikiwa. 1

18Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, 2 yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu. 1

19Jina lake tukufu lisifiwe milele, 2 ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen. 1

20Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.

← Psalms 71Read In The App, Free →Psalms 73 →

Study Psalms 72

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150