Psalms 40
1Nilimngoja Bwana kwa saburi, 2 naye akaniinamia, akasikia kilio changu. 1
2Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, 2 kutoka matope na utelezi; 1 akaiweka miguu yangu juu ya mwamba 2 na kunipa mahali imara pa kusimama. 1
3Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, 2 wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. 1 Wengi wataona na kuogopa 2 na kuweka tumaini lao kwa Bwana. 1
4Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, 2 asiyewategemea wenye kiburi, 2 wale wenye kugeukia miungu ya uongo. 1
5Ee Bwana Mungu wangu, 2 umefanya mambo mengi ya ajabu. 1 Mambo uliyopanga kwa ajili yetu 2 hakuna awezaye kukuhesabia; 1 kama ningesema na kuyaelezea, 2 yangekuwa mengi mno kuyaelezea. 1
6Dhabihu na sadaka hukuvitaka, 2 lakini umefungua masikio yangu; + 40:6 Au: bali mwili uliniandalia. 1 sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi 2 hukuzihitaji. 1
7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: 2 imeandikwa kunihusu katika kitabu. 1
8Ee Mungu wangu, 2 natamani kuyafanya mapenzi yako; 2 sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” 1
9Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, 2 sikufunga mdomo wangu, 2 Ee Bwana, kama ujuavyo. 1
10Sikuficha haki yako moyoni mwangu; 2 ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. 1 Sikuficha upendo wako na kweli yako 2 mbele ya kusanyiko kubwa. 1
11Ee Bwana, usizuilie huruma zako, 2 upendo wako na kweli yako daima vinilinde. 1
12Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, 2 dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. 1 Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, 2 nao moyo unazimia ndani yangu. 1
13Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa; 2 Ee Bwana, njoo hima unisaidie. 1
14Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, 2 waaibishwe na kufadhaishwa; 1 wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, 2 warudishwe nyuma kwa aibu. 1
15Wale waniambiao, “Aha! Aha!” 2 wafadhaishwe na iwe aibu yao. 1
16Lakini wote wakutafutao 2 washangilie na kukufurahia, 1 wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, 2 “ Bwana atukuzwe!” 1
17Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; 2 Bwana na anifikirie. 1 Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu; 2 Ee Mungu wangu, usikawie.