Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 29

1Mpeni Bwana, enyi mashujaa, 2 mpeni Bwana utukufu na nguvu. 1

2Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; 2 mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. 1

3Sauti ya Bwana iko juu ya maji; 2 Mungu wa utukufu hupiga radi, 2 Bwana hupiga radi juu ya maji makuu. 1

4Sauti ya Bwana ina nguvu; 2 sauti ya Bwana ni tukufu. 1

5Sauti ya Bwana huvunja mierezi; 2 Bwana huvunja vipande vipande 2 mierezi ya Lebanoni. 1

6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, 2 Sirioni + 29:6 Yaani Mlima Hermoni. urukaruke kama mwana nyati. 1

7Sauti ya Bwana hupiga kwa miali 2 ya umeme wa radi. 1

8Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; 2 Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi. 1

9Sauti ya Bwana huzalisha ayala, 2 na huuacha msitu wazi. 1 Hekaluni mwake wote wasema, 2 “Utukufu!” 1

10Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; 2 Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele. 1

11Bwana huwapa watu wake nguvu; 2 Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.

← Psalms 28Read In The App, Free →Psalms 30 →

Study Psalms 29

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150