Psalms 68
1Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike, 2 adui zake na wakimbie mbele zake. 1
2Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, 2 vivyo hivyo uwapeperushe mbali, 1 kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, 2 vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu. 1
3Bali wenye haki na wafurahi, 2 washangilie mbele za Mungu, 2 wafurahi na kushangilia. 1
4Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, 2 mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu: 1 jina lake ni Bwana, 2 furahini mbele zake. 1
5Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, 2 ni Mungu katika makao yake matakatifu. 1
6Mungu huwaweka wapweke katika jamaa, 2 huwaongoza wafungwa wakiimba, 2 bali waasi huishi katika nchi kame. 1
7Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako, 2 ulipopita nyikani, 1
8dunia ilitikisika, 2 mbingu zikanyesha mvua, 1 mbele za Mungu, Yule wa Sinai, 2 mbele za Mungu, Mungu wa Israeli. 1
9Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi 2 na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka. 1
10Ee Mungu, watu wako waliishi huko, 2 nawe kwa wingi wa utajiri wako 2 uliwapa maskini mahitaji yao. 1
11Bwana alitangaza neno, 2 waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa: 1
12“Wafalme na majeshi walikimbia upesi, 2 watu waliobaki kambini waligawana nyara. 1
13Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini, 2 mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha, 2 manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.” 1
14Wakati Mwenyezi + 68:14 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. alipowatawanya wafalme katika nchi, 2 ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni. 1
15Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka, 2 milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka. 1
16Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka, 2 kwa nini mnakazia macho kwa wivu, 1 katika mlima Mungu anaochagua kutawala, 2 ambako Bwana mwenyewe ataishi milele? 1
17Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu, 2 na maelfu ya maelfu; 1 Bwana amekuja kutoka Sinai 2 hadi katika patakatifu pake. 1
18Ulipopanda juu, uliteka mateka, 2 ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, 1 hata kutoka kwa wale walioasi, 2 ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko. 1
19Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, 2 ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. 1
20Mungu wetu ni Mungu aokoaye, 2 Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo. 1
21Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, 2 vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi. 1
22Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; 2 nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, 1
23ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, 2 huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.” 1
24Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, 2 maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, 2 yakielekea patakatifu pake. 1
25Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, 2 pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. 1
26Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, 2 msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli. 1
27Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza, 2 wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda, 2 hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali. 1
28Ee Mungu, amuru uwezo wako, 2 Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako, 2 kama ulivyofanya hapo awali. 1
29Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu 2 wafalme watakuletea zawadi. 1
30Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, 2 kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. 1 Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. 2 Tawanya mataifa yapendayo vita. 1
31Wajumbe watakuja kutoka Misri, 2 Kushi + 68:31 Kushi hapa ina maana maeneo ya Naili ya juu, yaani Ethiopia. atajisalimisha kwa Mungu. 1
32Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, 2 mwimbieni Bwana sifa, 1
33mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, 2 yeye angurumaye kwa sauti kuu. 1
34Tangazeni uwezo wa Mungu, 2 ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, 2 ambaye uwezo wake uko katika anga. 1
35Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, 2 Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. 1 Mungu Asifiwe!