Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 31

1Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, 2 usiache nikaaibika kamwe, 2 kwa haki yako uniokoe. 1

2Nitegee sikio lako, 2 uje uniokoe haraka; 1 uwe kwangu mwamba wa kimbilio, 2 ngome imara ya kuniokoa. 1

3Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, 2 uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako. 1

4Uniepushe na mtego niliotegewa, 2 maana wewe ndiwe kimbilio langu. 1

5Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, 2 unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli. 1

6Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili; 2 mimi ninamtumaini Bwana. 1

7Nitafurahia na kushangilia upendo wako, 2 kwa kuwa uliona mateso yangu 2 na ulijua maumivu ya nafsi yangu. 1

8Hukunikabidhi kwa adui yangu 2 bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi. 1

9Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; 2 macho yangu yanafifia kwa huzuni, 2 nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. 1

10Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, 2 naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; 1 nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, 2 na mifupa yangu inachakaa. 1

11Kwa sababu ya adui zangu wote, 2 nimedharauliwa kabisa na jirani zangu, 1 hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, 2 wale wanionao barabarani hunikimbia. 1

12Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa, 2 nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika. 1

13Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; 2 vitisho viko pande zote; 1 kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, 2 na kula njama kuniua. 1

14Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana; 2 nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” 1

15Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, 2 uniokoe mikononi mwa adui zangu 2 na wale wanifuatiao. 1

16Mwangazie mtumishi wako uso wako, 2 uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma. 1

17Usiniache niaibike, Ee Bwana, 2 kwa maana nimekulilia wewe, 1 bali waovu waaibishwe 2 na kunyamazishwa Kuzimu. 1

18Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, 2 kwa maana kwa kiburi na dharau 1 wao husema kwa majivuno 2 dhidi ya wenye haki. 1

19Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako, 2 uliowawekea akiba wakuchao, 1 ambao huwapa wale wakukimbiliao 2 machoni pa watu. 1

20Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako 2 kutokana na hila za wanadamu; 1 katika makao yako huwaweka salama 2 kutokana na ndimi za mashtaka. 1

21Atukuzwe Bwana, 2 kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu 2 nilipokuwa katika mji uliozingirwa. 1

22Katika hofu yangu nilisema, 2 “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” 1 Hata hivyo ulisikia kilio changu 2 ukanihurumia nilipokuita unisaidie. 1

23Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote! 2 Bwana huwahifadhi waaminifu, 2 lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu. 1

24Kuweni hodari na mjipe moyo, 2 ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.

← Psalms 30Read In The App, Free →Psalms 32 →

Study Psalms 31

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150