Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 2

1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, 2 na kabila za watu kula njama bure? 1

2Wafalme wa dunia wanajipanga 2 na watawala wanajikusanya pamoja 1 dhidi ya Bwana 2 na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. 1

3Wanasema, “Tuvunje minyororo yao 2 na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” 1

4Yeye atawalaye mbinguni hucheka, 2 Bwana huwadharau. 1

5Kisha huwakemea katika hasira yake 2 na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, 1

6“Nimemtawaza Mfalme wangu 2 juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” 1 Ushindi Wa Mfalme 1

7Nitatangaza amri ya Bwana: 2 Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, 2 leo mimi nimekuzaa. 1

8Niombe, nami nitayafanya mataifa 2 kuwa urithi wako, 2 miisho ya dunia kuwa milki yako. 1

9Utawatawala kwa fimbo ya chuma 2 na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” 1

10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; 2 mwonyeke, enyi watawala wa dunia. 1

11Mtumikieni Bwana kwa hofu 2 na mshangilie kwa kutetemeka. 1

12Mbusu Mwana, asije akakasirika 2 nawe ukaangamizwa katika njia yako, 1 kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. 2 Heri wote wanaomkimbilia.

← Psalms 1Read In The App, Free →Psalms 3 →

Study Psalms 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150