Psalms 63
1Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, 2 nakutafuta kwa moyo wote; 1 nafsi yangu inakuonea kiu, 2 mwili wangu unakuonea wewe shauku, 1 katika nchi kame na iliyochoka 2 mahali ambapo hapana maji. 1
2Nimekuona katika mahali patakatifu 2 na kuuona uwezo wako na utukufu wako. 1
3Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, 2 midomo yangu itakuadhimisha. 1
4Nitakusifu siku zote za maisha yangu, 2 na kwa jina lako nitainua mikono yangu. 1
5Nafsi yangu itatoshelezwa 2 kama kwa wingi wa vyakula; 1 kwa midomo iimbayo 2 kinywa changu kitakusifu wewe. 1
6Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, 2 ninawaza juu yako makesha yote ya usiku. 1
7Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, 2 chini ya uvuli wa mbawa zako naimba. 1
8Nafsi yangu inaambatana nawe, 2 mkono wako wa kuume hunishika. 1
9Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa, 2 watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia. 1
10Watatolewa wafe kwa upanga, 2 nao watakuwa chakula cha mbweha. 1
11Bali mfalme atafurahi katika Mungu, 2 wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, 2 bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.