Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 92

1Ni vyema kumshukuru Bwana 2 na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana, 1

2kuutangaza upendo wako asubuhi, 2 na uaminifu wako wakati wa usiku, 1

3kwa zeze yenye nyuzi kumi 2 na kwa sauti ya kinubi. 1

4Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, 2 nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako. 1

5Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, 2 tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako! 1

6Mjinga hafahamu, 2 mpumbavu haelewi, 1

7ingawa waovu huchipua kama majani 2 na wote watendao mabaya wanastawi, 2 wataangamizwa milele. 1

8Bali wewe, Ee Bwana, 2 utatukuzwa milele. 1

9Ee Bwana, hakika adui zako, 2 hakika adui zako wataangamia. 2 Wote watendao mabaya watatawanyika. 1

10Umeitukuza pembe + 92:10 Pembe inawakilisha nguvu. yangu kama ile ya nyati dume, 2 mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu. 1

11Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, 2 masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu. 1

12Wenye haki watastawi kama mtende, 2 watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni, 1

13waliopandwa katika nyumba ya Bwana, 2 watastawi katika nyua za Mungu wetu. 1

14Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, 2 watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, 1

15wakitangaza, “ Bwana ni mkamilifu; 2 yeye ni Mwamba wangu, 2 na ndani yake hamna uovu.”

← Psalms 91Read In The App, Free →Psalms 93 →

Study Psalms 92

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150