Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 32

1Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, 2 ambaye dhambi zake zimefunikwa. 1

2Heri mtu yule ambaye Bwana 2 hamhesabii dhambi, 1 na ambaye rohoni mwake 2 hamna udanganyifu. 1

3Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa 2 kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa. 1

4Usiku na mchana 2 mkono wako ulinilemea, 1 nguvu zangu zilinyonywa 2 kama vile katika joto la kiangazi. 1

5Kisha nilikujulisha dhambi yangu 2 wala sikuficha uovu wangu. 1 Nilisema, “Nitaungama 2 makosa yangu kwa Bwana.” 1 Ndipo uliponisamehe 2 hatia ya dhambi yangu. 1

6Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe 2 wakati unapopatikana, 1 hakika maji makuu yatakapofurika 2 hayatamfikia yeye. 1

7Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, 2 utaniepusha na taabu 2 na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. 1

8Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; 2 nitakushauri na kukuangalia. 1

9Usiwe kama farasi au nyumbu 2 wasio na akili, 1 ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu 2 la sivyo hawatakukaribia. 1

10Mtu mwovu ana taabu nyingi, 2 bali upendo usio na kikomo wa Bwana 2 unamzunguka mtu anayemtumaini. 1

11Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki! 2 Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!

← Psalms 31Read In The App, Free →Psalms 33 →

Study Psalms 32

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150