Psalms 148
1Msifuni Bwana. 1 Msifuni Bwana kutoka mbinguni, 2 msifuni juu vileleni. 1
2Msifuni, enyi malaika wake wote, 2 msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. 1
3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, 2 msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo. 1
4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, 2 na ninyi maji juu ya anga. 1
5Vilisifu jina la Bwana 2 kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa. 1
6Aliviweka mahali pake milele na milele, 2 alitoa amri ambayo haibadiliki milele. 1
7Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, 2 ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari, 1
8umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, 2 pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, 1
9ninyi milima na vilima vyote, 2 miti ya matunda na mierezi yote, 1
10wanyama wa mwituni na mifugo yote, 2 viumbe vidogo na ndege warukao, 1
11wafalme wa dunia na mataifa yote, 2 ninyi wakuu na watawala wote wa dunia, 1
12wanaume vijana na wanawali, 2 wazee na watoto. 1
13Wote na walisifu jina la Bwana, 2 kwa maana jina lake pekee limetukuka, 2 utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. 1
14Amewainulia watu wake pembe, + 148:14 Pembe hapa inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme. 2 sifa ya watakatifu wake wote, 2 ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. 1 Msifuni Bwana.