Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 55

1Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, 2 wala usidharau hoja yangu. 1

2Nisikie na unijibu. 1 Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa 1

3kwa sauti ya adui, 2 kwa kukaziwa macho na waovu, 1 kwa sababu wananiletea mateso juu yangu 2 na kunitukana kwa hasira zao. 1

4Moyo wangu umejaa uchungu, 2 hofu ya kifo imenishambulia. 1

5Woga na kutetemeka vimenizunguka, 2 hofu kuu imenigharikisha. 1

6Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! 2 Ningeruka niende mbali kupumzika. 1

7Ningalitorokea mbali sana 2 na kukaa jangwani, 1

8ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, 2 mbali na tufani kali na dhoruba.” 1

9Ee Bwana, uwatahayarishe waovu 2 na uwachanganyishie semi zao, 2 maana nimeona jeuri na ugomvi mjini. 1

10Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, 2 uovu na dhuluma vimo ndani yake. 1

11Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini, 2 vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake. 1

12Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia, 2 kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, 2 ningejificha asinione. 1

13Kumbe ni wewe, mwenzangu, 2 mshiriki na rafiki yangu wa karibu, 1

14ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri, 2 tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu. 1

15Kifo na kiwajie adui zangu ghafula, 2 na washuke kuzimu wangali hai, 2 kwa maana uovu upo ndani yao. 1

16Lakini ninamwita Mungu, 2 naye Bwana huniokoa. 1

17Jioni, asubuhi na adhuhuri 2 ninalia kwa huzuni, 2 naye husikia sauti yangu. 1

18Huniokoa nikawa salama katika vita 2 vilivyopangwa dhidi yangu, 2 ingawa watu wengi hunipinga. 1

19Mungu anayemiliki milele, 2 atawasikia na kuwaadhibu, 1 watu ambao hawabadilishi njia zao, 2 wala hawana hofu ya Mungu. 1

20Mwenzangu hushambulia rafiki zake, 2 naye huvunja agano lake. 1

21Mazungumzo yake ni laini kama siagi, 2 hata hivyo vita vimo moyoni mwake. 1 Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, 2 hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. 1

22Mtwike Bwana fadhaa zako, 2 naye atakutegemeza, 2 hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke. 1

23Lakini wewe, Ee Mungu, 2 utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. 1 Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, 2 hawataishi nusu ya siku zao. 1 Lakini mimi ninakutumaini wewe.

← Psalms 54Read In The App, Free →Psalms 56 →

Study Psalms 55

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150