Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 18

1Nakupenda wewe, Ee Bwana, 2 nguvu yangu. 1

2Bwana ni mwamba wangu, 2 ngome yangu na mwokozi wangu, 1 Mungu wangu ni mwamba, 2 ambaye kwake ninakimbilia. 1 Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, 2 ngome yangu. 1

3Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa, 2 nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. 1

4Kamba za mauti zilinizunguka, 2 mafuriko ya maangamizi yalinilemea. 1

5Kamba za kuzimu zilinizunguka, 2 mitego ya mauti ilinikabili. 1

6Katika shida yangu nalimwita Bwana, 2 nilimlilia Mungu wangu anisaidie. 1 Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, 2 kilio changu kikafika mbele zake, 2 masikioni mwake. 1

7Dunia ilitetemeka na kutikisika, 2 misingi ya milima ikatikisika, 2 vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. 1

8Moshi ukapanda kutoka puani mwake, 2 moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, 1 makaa ya moto yawakayo 2 yakatoka ndani mwake. 1

9Akazipasua mbingu akashuka chini, 2 mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 1

10Alipanda juu ya kerubi akaruka, 2 akapaa juu kwa mbawa za upepo. 1

11Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, 2 hema lake kumzunguka, 2 mawingu meusi ya mvua ya angani. 1

12Kutokana na mwanga wa uwepo wake 2 mawingu yalisogea, 1 ikanyesha mvua ya mawe 2 na umeme wa radi. 1

13Bwana alinguruma kutoka mbinguni, 2 sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. 1

14Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, 2 naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza. 1

15Mabonde ya bahari yalifunuliwa, 2 na misingi ya dunia ikawa wazi 1 kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, 2 kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako. 1

16Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; 2 alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. 1

17Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, 2 kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. 1

18Walinikabili siku ya msiba wangu, 2 lakini Bwana alikuwa msaada wangu. 1

19Alinileta nje mahali penye nafasi tele, 2 akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. 1

20Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; 2 sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. 1

21Kwa maana nimezishika njia za Bwana; 2 sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. 1

22Sheria zake zote zi mbele yangu, 2 wala sijayaacha maagizo yake. 1

23Nimekuwa sina hatia mbele zake, 2 nami nimejilinda nisitende dhambi. 1

24Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; 2 sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake. 1

25Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu, 2 kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia. 1

26Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, 2 lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi. 1

27Wewe huwaokoa wanyenyekevu, 2 lakini huwashusha wenye kiburi. 1

28Wewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka; 2 Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga. 1

29Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, 2 nikiwa pamoja na Mungu wangu 2 nitaweza kuruka ukuta. 1

30Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, 2 neno la Bwana halina dosari. 1 Yeye ni ngao kwa wote 2 wanaokimbilia kwake. 1

31Kwa maana ni nani aliye Mungu 2 zaidi ya Bwana? 1 Ni nani aliye Mwamba 2 isipokuwa Mungu wetu? 1

32Mungu ndiye anivikaye nguvu 2 na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. 1

33Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, 2 huniwezesha kusimama mahali palipo juu. 1

34Huifundisha mikono yangu kupigana vita; 2 mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. 1

35Hunipa ngao yako ya ushindi, 2 nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, 2 unajishusha chini ili kuniinua. 1

36Huyapanua mapito yangu, 2 ili miguu yangu isiteleze. 1

37Niliwafuatia adui zangu na nikawapata, 2 sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa. 1

38Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena; 2 walianguka chini ya miguu yangu. 1

39Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; 2 uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. 1

40Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, 2 nami nikawaangamiza adui zangu. 1

41Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; 2 walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu. 1

42Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo; 2 niliwamwaga nje kama tope barabarani. 1

43Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu; 2 umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa, 2 watu ambao sikuwajua wananitumikia. 1

44Mara wanisikiapo hunitii, 2 wageni hunyenyekea mbele yangu. 1

45Wote wanalegea, 2 wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. 1

46Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! 2 Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu! 1

47Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, 2 awatiishaye mataifa chini yangu, 2

48aniokoaye na adui zangu. 1 Uliniinua juu ya adui zangu; 2 uliniokoa toka kwa watu wajeuri. 1

49Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana; 2 nitaliimbia sifa jina lako. 1

50Humpa mfalme wake ushindi mkuu, 2 huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, 2 kwa Daudi na wazao wake milele.

← Psalms 17Read In The App, Free →Psalms 19 →

Study Psalms 18

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150