Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 27

1Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, 2 nimwogope nani? 1 Bwana ni ngome ya uzima wangu, 2 nimhofu nani? 1

2Waovu watakaposogea dhidi yangu 2 ili wanile nyama yangu, 1 adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia, 2 watajikwaa na kuanguka. 1

3Hata jeshi linizunguke pande zote, 2 moyo wangu hautaogopa; 1 hata vita vitokee dhidi yangu, 2 hata hapo nitakuwa na ujasiri. 1

4Jambo moja ninamwomba Bwana, 2 hili ndilo ninalolitafuta: 1 niweze kukaa nyumbani mwa Bwana 2 siku zote za maisha yangu, 1 niutazame uzuri wa Bwana 2 na kumtafuta hekaluni mwake. 1

5Kwa kuwa siku ya shida, 2 atanihifadhi salama katika maskani yake, 1 atanificha uvulini mwa hema yake 2 na kuniweka juu kwenye mwamba. 1

6Kisha kichwa changu kitainuliwa 2 juu ya adui zangu wanaonizunguka. 1 Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; 2 nitamwimbia Bwana na kumsifu. 1

7Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, 2 unihurumie na unijibu. 1

8Moyo wangu unasema kuhusu wewe, 2 “Utafute uso wake!” 2 Uso wako, Bwana “Nitautafuta.” 1

9Usinifiche uso wako, 2 usimkatae mtumishi wako kwa hasira; 2 wewe umekuwa msaada wangu. 1 Usinikatae wala usiniache, 2 Ee Mungu Mwokozi wangu. 1

10Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, 2 Bwana atanipokea. 1

11Nifundishe njia yako, Ee Bwana, 2 niongoze katika njia iliyonyooka 2 kwa sababu ya watesi wangu. 1

12Usiniachilie kwa nia za adui zangu, 2 kwa maana mashahidi wa uongo 2 wameinuka dhidi yangu, 2 wakipumua ujeuri. 1

13Nami bado nina tumaini hili: 2 nitauona wema wa Bwana 2 katika nchi ya walio hai. 1

14Mngojee Bwana, 2 uwe hodari na mwenye moyo mkuu, 2 nawe, umngojee Bwana.

← Psalms 26Read In The App, Free →Psalms 28 →

Study Psalms 27

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150