Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 91

1Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, 2 atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. + 91:1 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. 1

2Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, 2 Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” 1

3Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, 2 na maradhi ya kuambukiza ya kuua. 1

4Atakufunika kwa manyoya yake, 2 chini ya mbawa zake utapata kimbilio, 2 uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. 1

5Hutaogopa vitisho vya usiku, 2 wala mshale urukao mchana, 1

6wala maradhi ya kuambukiza 2 yanayonyemelea gizani, 2 wala tauni iharibuyo adhuhuri. 1

7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, 2 kumi elfu mkono wako wa kuume, 2 lakini haitakukaribia wewe. 1

8Utatazama tu kwa macho yako 2 na kuona adhabu ya waovu. 1

9Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: 2 naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu, 1

10basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, 2 hakuna maafa yataikaribia hema yako. 1

11Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, 2 wakulinde katika njia zako zote. 1

12Mikononi mwao watakuinua, 2 ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe. 1

13Utawakanyaga simba na nyoka wakali, 2 simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. 1

14Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; 2 nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu. 1

15Ataniita, nami nitamjibu; 2 nitakuwa pamoja naye katika taabu, 2 nitamwokoa na kumheshimu. 1

16Kwa siku nyingi nitamshibisha 2 na kumwonyesha wokovu wangu.”

← Psalms 90Read In The App, Free →Psalms 92 →

Study Psalms 91

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150