Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 7

1Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, 2 uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, 1

2la sivyo watanirarua kama simba 2 na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. 1

3Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya 2 na kuna hatia mikononi mwangu, 1

4au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, 2 au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu, 1

5basi adui anifuatie na kunipata, 2 auponde uhai wangu ardhini 2 na kunilaza mavumbini. 1

6Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, 2 inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. 2 Amka, Mungu wangu, uamue haki. 1

7Kusanyiko la watu na likuzunguke. 2 Watawale kutoka juu. 2

8Bwana na awahukumu kabila za watu. 1 Nihukumu Ee Bwana, 2 kwa kadiri ya haki yangu, 1 kwa kadiri ya uadilifu wangu, 2 Ewe Uliye Juu Sana. 1

9Ee Mungu mwenye haki, 2 uchunguzaye mawazo na mioyo, 1 komesha ghasia za waovu 2 na ufanye wenye haki waishi kwa amani. 1

10Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, 2 awaokoaye wanyofu wa moyo. 1

11Mungu ni mwamuzi mwenye haki, 2 Mungu aghadhibikaye kila siku. 1

12Kama hakutuhurumia, 2 atanoa upanga wake, 2 ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. 1

13Ameandaa silaha zake kali, 2 ameweka tayari mishale yake ya moto. 1

14Yeye aliye na mimba ya uovu 2 na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo. 1

15Yeye achimbaye shimo na kulifukua 2 hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. 1

16Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, 2 ukatili wake humrudia kichwani. 1

17Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, 2 na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.

← Psalms 6Read In The App, Free →Psalms 8 →

Study Psalms 7

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150