Psalms 28
1Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; 2 usiwe kwangu kama kiziwi. 1 Kwa sababu ukinyamaza 2 nitafanana na walioshuka shimoni. 1
2Sikia kilio changu unihurumie 2 ninapokuita kwa ajili ya msaada, 1 niinuapo mikono yangu kuelekea 2 Patakatifu pa Patakatifu pako. 1
3Usiniburute pamoja na waovu, 2 pamoja na hao watendao mabaya, 1 ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, 2 lakini mioyoni mwao wameficha chuki. 1
4Walipe sawasawa na matendo yao, 2 sawasawa na matendo yao maovu; 1 walipe sawasawa na kazi za mikono yao, 2 uwalipe wanavyostahili. 1
5Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, 2 na yale ambayo mikono yake imetenda, 1 atawabomoa na kamwe 2 hatawajenga tena. 1
6Bwana asifiwe, 2 kwa maana amesikia kilio changu 2 nikimwomba anihurumie. 1
7Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, 2 moyo wangu umemtumaini yeye, 2 nami nimesaidiwa. 1 Moyo wangu unarukaruka kwa furaha 2 nami nitamshukuru kwa wimbo. 1
8Bwana ni nguvu ya watu wake, 2 ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake. 1
9Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; 2 uwe mchungaji wao na uwabebe milele.