Psalms 64
1Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu, 2 uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui. 1
2Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu, 2 kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya. 1
3Wananoa ndimi zao kama panga 2 na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. 1
4Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, 2 humrushia ghafula bila woga. 1
5Kila mmoja humtia moyo mwenzake 2 katika mipango mibaya; 1 huzungumza juu ya kuficha mitego yao, 2 nao husema, “Ni nani ataiona?” 1
6Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema, 2 “Tumebuni mpango mkamilifu!” 2 Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila. 1
7Bali Mungu atawapiga kwa mishale, 2 nao ghafula wataangushwa. 1
8Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao 2 na kuwaleta kwenye maangamizi; 1 wote wawaonao watatikisa vichwa vyao 2 kwa dharau. 1
9Wanadamu wote wataogopa, 2 watatangaza kazi za Mungu 2 na kutafakari yale aliyoyatenda. 1
10Wenye haki na wafurahi katika Bwana, 2 na wakimbilie kwake; 2 wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye!