Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 116

1Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; 2 amesikia kilio changu ili anihurumie. 1

2Kwa sababu amenitegea sikio lake, 2 nitamwita siku zote za maisha yangu. 1

3Kamba za mauti zilinizunguka, 2 maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, 2 nikalemewa na taabu na huzuni. 1

4Ndipo nikaliitia jina la Bwana: 2 “Ee Bwana, niokoe!” 1

5Bwana ni mwenye neema na haki, 2 Mungu wetu ni mwingi wa huruma. 1

6Bwana huwalinda wanyenyekevu, 2 nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. 1

7Ee nafsi yangu, tulia tena, 2 kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako. 1

8Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, 2 umeniokoa nafsi yangu na mauti, 1 macho yangu kutokana na machozi, 2 miguu yangu kutokana na kujikwaa, 1

9ili niweze kutembea mbele za Bwana, 2 katika nchi ya walio hai. 1

10Niliamini, kwa hiyo nilisema, 2 “Mimi nimeteseka sana.” 1

11Katika taabu yangu nilisema, 2 “Wanadamu wote ni waongo.” 1

12Nimrudishie Bwana nini 2 kwa wema wake wote alionitendea? 1

13Nitakiinua kikombe cha wokovu 2 na kulitangaza jina la Bwana. 1

14Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana 2 mbele za watu wake wote. 1

15Kifo cha watakatifu kina thamani 2 machoni pa Bwana. 1

16Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, 2 mimi ni mtumishi wako, 2 mwana wa mjakazi wako; + 116:16 Au: mwanao mwaminifu. 1 umeniweka huru 2 toka katika minyororo yangu. 1

17Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru 2 na kuliita jina la Bwana. 1

18Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana 2 mbele za watu wake wote, 1

19katika nyua za nyumba ya Bwana, 2 katikati yako, ee Yerusalemu. 2 Msifuni Bwana.

← Psalms 115Read In The App, Free →Psalms 117 →

Study Psalms 116

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150