Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 103

1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. 2 Vyote vilivyomo ndani yangu 2 vilihimidi jina lake takatifu. 1

2Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, 2 wala usisahau wema wake wote, 1

3akusamehe dhambi zako zote, 2 akuponya magonjwa yako yote, 1

4aukomboa uhai wako na kaburi, 2 akuvika taji ya upendo na huruma, 1

5atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, 2 ili ujana wako uhuishwe kama wa tai. 1

6Bwana hutenda haki, 2 naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa. 1

7Alijulisha Mose njia zake, 2 na wana wa Israeli matendo yake. 1

8Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; 2 si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo. 1

9Yeye hatalaumu siku zote, 2 wala haweki hasira yake milele, 1

10yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu 2 wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. 1

11Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana, 2 ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; 1

12kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, 2 ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi. 1

13Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, 2 ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha; 1

14kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, 2 anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi. 1

15Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, 2 anachanua kama ua la shambani; 1

16upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, 2 mahali pake hapalikumbuki tena. 1

17Lakini kutoka milele hata milele 2 upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, 2 nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: 1

18kwa wale walishikao agano lake 2 na kukumbuka kuyatii mausia yake. 1

19Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, 2 ufalme wake unatawala juu ya vyote. 1

20Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, 2 ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, 2 ninyi mnaotii neno lake. 1

21Mhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, 2 ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. 1

22Mhimidini Bwana, kazi zake zote 2 kila mahali katika milki yake. 1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

← Psalms 102Read In The App, Free →Psalms 104 →

Study Psalms 103

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150