Psalms 26
1Ee Bwana, nithibitishe katika haki, 2 maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; 1 nimemtumainia Bwana 2 bila kusitasita. 1
2Ee Bwana, unijaribu, unipime, 2 uuchunguze moyo wangu 2 na mawazo yangu; 1
3kwa maana upendo wako 2 uko mbele yangu daima, 1 nami natembea siku zote 2 katika kweli yako. 1
4Siketi pamoja na watu wadanganyifu, 2 wala siandamani na wanafiki, 1
5ninachukia kusanyiko la watenda mabaya 2 na ninakataa kuketi pamoja na waovu. 1
6Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, 2 naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana, 1
7nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, 2 huku nikisimulia matendo yako ya ajabu. 1
8Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi, 2 mahali ambapo utukufu wako hukaa. 1
9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi, 2 wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu, 1
10ambao mikononi mwao kuna mipango miovu, 2 ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa. 1
11Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; 2 nikomboe na unihurumie. 1
12Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; 2 katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.