Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 35

1Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami, 2 upigane na hao wanaopigana nami. 1

2Chukua ngao na kigao. 2 Inuka unisaidie. 1

3Inua mkuki wako na fumo + 35:3 Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi. lako 2 dhidi ya hao wanaonifuatia. 1 Iambie nafsi yangu, 2 “Mimi ni wokovu wako.” 1

4Wafedheheshwe na waaibishwe 2 wale wanaotafuta uhai wangu. 1 Wanaofanya shauri kuniangamiza 2 warudishwe nyuma kwa hofu. 1

5Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo, 2 malaika wa Bwana akiwafukuza. 1

6Njia yao na iwe giza na ya utelezi, 2 malaika wa Bwana akiwafuatilia. 1

7Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu, 2 na bila sababu wamenichimbia shimo, 1

8maafa na yawapate ghafula: 2 wavu walionifichia na uwatege wenyewe, 1 na waanguke katika shimo hilo, 2 kwa maangamizo yao. 1

9Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana 2 na kuufurahia wokovu wake. 1

10Nitapaza sauti yangu nikisema, 2 “Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana? 1 Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao, 2 maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!” 1

11Mashahidi wakatili wanainuka, 2 wananiuliza mambo nisiyoyajua. 1

12Wananilipa baya kwa jema 2 na kuiacha nafsi yangu ukiwa. 1

13Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia 2 na nikajinyenyekesha kwa kufunga. 1 Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa, 2

14niliendelea kuomboleza 2 kama vile wao ni rafiki au ndugu. 1 Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni 2 kama ninayemwombolezea mama yangu. 1

15Lakini nilipojikwaa, 2 walikusanyika kwa shangwe; 1 washambuliaji walijikusanya dhidi yangu 2 bila mimi kujua. 2 Walinisingizia pasipo kukoma. 1

16Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki, 2 wamenisagia meno. 1

17Ee Bwana, utatazama mpaka lini? 2 Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, 1 uhai wangu wa thamani 2 kutokana na simba hawa. 1

18Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, 2 nitakusifu katikati ya watu wengi. 1

19Usiwaache wale wanaonisimanga, 2 wale ambao ni adui zangu bila sababu; 1 usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu 2 wakonyeze jicho kwa hila. 1

20Hawazungumzi kwa amani, 2 bali wanatunga mashtaka ya uongo 1 dhidi ya wale wanaoishi 2 kwa utulivu katika nchi. 1

21Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha! 2 Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.” 1

22Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya. 2 Usiwe mbali nami, Ee Bwana. 1

23Amka, inuka unitetee! 2 Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu. 1

24Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu, 2 sawasawa na haki yako; 2 usiwaache wakusimange. 1

25Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” 2 Au waseme, “Tumemmeza.” 1

26Wote wanaofurahia dhiki yangu 2 waaibishwe na wachanganyikiwe; 1 hao wanaojiinua dhidi yangu 2 wavikwe aibu na dharau. 1

27Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki 2 wapige kelele za shangwe na furaha; 1 hebu waseme siku zote, “ Bwana atukuzwe, 2 ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.” 1

28Ulimi wangu utanena haki yako 2 na sifa zako mchana kutwa.

← Psalms 34Read In The App, Free →Psalms 36 →

Study Psalms 35

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150