Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 69

1Ee Mungu, niokoe, 2 kwa maana maji yamenifika shingoni. 1

2Ninazama kwenye vilindi vya matope, 2 pasipo mahali pa kukanyaga, 1 Nimefika kwenye maji makuu, 2 mafuriko yamenigharikisha. 1

3Nimechoka kwa kuomba msaada, 2 koo langu limekauka. 1 Macho yangu yanafifia, 2 nikimtafuta Mungu wangu. 1

4Wale wanaonichukia bila sababu 2 ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; 1 wengi ni adui kwangu bila sababu, 2 wale wanaotafuta kuniangamiza. 1 Ninalazimishwa kurudisha 2 kitu ambacho sikuiba. 1

5Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, 2 wala hatia yangu haikufichika kwako. 1

6Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 wakutumainio wasiaibishwe 2 kwa ajili yangu; 1 wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, 2 Ee Mungu wa Israeli. 1

7Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, 2 aibu imefunika uso wangu. 1

8Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, 2 mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. 1

9Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, 2 matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. 1

10Ninapolia na kufunga, 2 lazima nivumilie matusi. 1

11Ninapovaa nguo ya gunia, 2 watu hunidharau. 1

12Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, 2 nimekuwa wimbo wa walevi. 1

13Lakini Ee Bwana, ninakuomba, 2 kwa wakati ukupendezao; 1 katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, 2 unijibu kwa wokovu wako wa hakika. 1

14Uniokoe katika matope, 2 usiniache nizame; 1 niokoe na hao wanichukiao, 2 kutoka kwenye vilindi vya maji. 1

15Usiache mafuriko yanigharikishe 2 au vilindi vinimeze, 2 au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. 1

16Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; 2 kwa huruma zako nyingi unigeukie. 1

17Usimfiche mtumishi wako uso wako, 2 uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. 1

18Njoo karibu uniokoe, 2 nikomboe kwa sababu ya adui zangu. 1

19Unajua jinsi ninavyodharauliwa, 2 kufedheheshwa na kuaibishwa, 2 adui zangu wote unawajua. 1

20Dharau zimenivunja moyo 2 na nimekata tamaa, 1 nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, 2 wa kunituliza, lakini sikumpata. 1

21Waliweka nyongo katika chakula changu 2 na walinipa siki nilipokuwa na kiu. 1

22Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, 2 nayo iwe upatilizo na tanzi. 1

23Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, 2 nayo migongo yao iinamishwe daima. 1

24Uwamwagie ghadhabu yako, 2 hasira yako kali na iwapate. 1

25Mahali pao na pawe ukiwa, 2 wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. 1

26Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, 2 na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza. 1

27Walipize uovu juu ya uovu, 2 usiwaache washiriki katika wokovu wako. 1

28Wafutwe kutoka kitabu cha uzima 2 na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki. 1

29Mimi niko katika maumivu na dhiki; 2 Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. 1

30Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, 2 nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani. 1

31Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, 2 zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. 1

32Maskini wataona na kufurahi: 2 ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi! 1

33Bwana huwasikia wahitaji 2 wala hadharau watu wake waliotekwa. 1

34Mbingu na dunia zimsifu, 2 bahari na vyote viendavyo ndani yake, 1

35kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni 2 na kuijenga tena miji ya Yuda. 1 Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, 2

36watoto wa watumishi wake watairithi 1 na wale wote walipendao jina lake 2 wataishi humo.

← Psalms 68Read In The App, Free →Psalms 70 →

Study Psalms 69

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150