Psalms 83
1Ee Mungu, usinyamaze kimya, 2 usinyamaze, Ee Mungu, usitulie. 1
2Tazama watesi wako wanafanya fujo, 2 jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao. 1
3Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, 2 wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda. 1
4Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, 2 ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.” 1
5Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, 2 wanafanya muungano dhidi yako, 1
6mahema ya Edomu na Waishmaeli, 2 ya Wamoabu na Wahagari, 1
7Gebali, + 83:7 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). Amoni na Amaleki, 2 Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro. 1
8Hata Ashuru wameungana nao 2 kuwapa nguvu wazao wa Loti. 1
9Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, 2 na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini 2 hapo kijito cha Kishoni, 1
10ambao waliangamia huko Endori 2 na wakawa kama takataka juu ya nchi. 1
11Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, 2 watawala wao kama Zeba na Salmuna, 1
12ambao walisema, “Na tumiliki nchi 2 ya malisho ya Mungu.” 1
13Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, 2 kama makapi yapeperushwayo na upepo. 1
14Kama vile moto uteketezavyo msitu 2 au mwali wa moto unavyounguza milima, 1
15wafuatilie kwa tufani yako 2 na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako. 1
16Funika nyuso zao kwa aibu 2 ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana. 1
17Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, 2 na waangamie kwa aibu. 1
18Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, 2 kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.