Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 95

1Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; 2 tumfanyie kelele za shangwe 2 Mwamba wa wokovu wetu. 1

2Tuje mbele zake kwa shukrani, 2 tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. 1

3Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, 2 mfalme mkuu juu ya miungu yote. 1

4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, 2 na vilele vya milima ni mali yake. 1

5Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, 2 na mikono yake iliumba nchi kavu. 1

6Njooni, tusujudu, tumwabudu, 2 tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu, 1

7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, 2 na sisi ni watu wa malisho yake, 2 kondoo chini ya utunzaji wake. 1 Kama mkiisikia sauti yake leo, 2

8msiifanye mioyo yenu migumu 2 kama mlivyofanya kule Meriba, + 95:8 Meriba maana yake ni Kugombana. 1 kama mlivyofanya siku ile 2 kule Masa + 95:8 Masa maana yake ni Kujaribiwa. jangwani, 1

9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, 2 ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu. 1

10Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile, 2 nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka, 2 nao hawajazijua njia zangu.” 1

11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, 2 “Kamwe hawataingia rahani mwangu.”

← Psalms 94Read In The App, Free →Psalms 96 →

Study Psalms 95

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150