Psalms 16
1Ee Mungu, uniweke salama, 2 kwa maana kwako nimekimbilia. 1
2Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; 2 pasipo wewe sina jambo jema.” 1
3Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, 2 ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. 1
4Huzuni itaongezeka kwa wale 2 wanaokimbilia miungu mingine. 1 Sitazimimina sadaka zao za damu 2 au kutaja majina yao midomoni mwangu. 1
5Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; 2 umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. 1
6Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, 2 hakika nimepata urithi mzuri. 1
7Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, 2 hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha. 1
8Nimemweka Bwana mbele yangu daima. 2 Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, 2 sitatikisika. 1
9Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; 2 mwili wangu nao utapumzika salama, 1
10kwa maana hutaniacha kaburini, 2 wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu. 1
11Umenijulisha njia ya uzima; 2 utanijaza na furaha mbele zako, 1 pamoja na furaha za milele 2 katika mkono wako wa kuume.