Psalms 19
1Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, 2 anga zahubiri kazi ya mikono yake. 1
2Siku baada ya siku zinatoa habari, 2 usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. 1
3Hakuna msemo wala lugha, 2 ambapo sauti zao hazisikiki. 1
4Sauti yao imeenea duniani pote, 2 nayo maneno yao yameenea 2 hadi miisho ya ulimwengu. 1 Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua, 2
5linafanana na bwana arusi 2 akitoka chumbani mwake, 1 kama shujaa afurahiavyo 2 kukamilisha kushindana kwake. 1
6Huchomoza upande mmoja wa mbingu, 2 na kufanya mzunguko wake 2 hadi upande mwingine. 2 Hakuna kilichojificha joto lake. 1
7Sheria ya Bwana ni kamilifu, 2 ikihuisha nafsi. 1 Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, 2 zikimpa mjinga hekima. 1
8Maagizo ya Bwana ni kamili, 2 nayo hufurahisha moyo. 1 Amri za Bwana huangaza, 2 zatia nuru machoni. 1
9Kumcha Bwana ni utakatifu, 2 nako kwadumu milele. 1 Amri za Bwana ni za hakika, 2 nazo zina haki. 1
10Ni za thamani kuliko dhahabu, 2 kuliko dhahabu iliyo safi sana, 1 ni tamu kuliko asali, 2 kuliko asali kutoka kwenye sega. 1
11Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, 2 katika kuzishika kuna thawabu kubwa. 1
12Ni nani awezaye kutambua makosa yake? 2 Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. 1
13Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, 2 nazo zisinitawale. 1 Ndipo nitakapokuwa sina lawama, 2 wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa. 1
14Maneno ya kinywa changu 2 na mawazo ya moyo wangu, 1 yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, 2 Mwamba wangu na Mkombozi wangu.