Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 21

1Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. 2 Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake 2 kwa ushindi unaompa! 1

2Umempa haja ya moyo wake 2 na hukumzuilia maombi ya midomo yake. 1

3Ulimkaribisha kwa baraka tele 2 na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. 1

4Alikuomba maisha, nawe ukampa, 2 wingi wa siku milele na milele. 1

5Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, 2 umeweka juu yake fahari na utukufu. 1

6Hakika umempa baraka za milele, 2 umemfanya awe na furaha 2 kwa shangwe ya uwepo wako. 1

7Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; 2 kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. 1

8Mkono wako utawashika adui zako wote, 2 mkono wako wa kuume utawakamata adui zako. 1

9Wakati utakapojitokeza 2 utawafanya kama tanuru ya moto. 1 Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, 2 moto wake utawateketeza. 1

10Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, 2 uzao wao kutoka wanadamu. 1

11Ingawa watapanga mabaya dhidi yako 2 na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa, 1

12kwa kuwa utawafanya wakimbie 2 utakapowalenga usoni pao 2 kwa mshale kutoka kwenye upinde wako. 1

13Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, 2 tutaimba na kusifu nguvu zako.

← Psalms 20Read In The App, Free →Psalms 22 →

Study Psalms 21

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150