Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 34

1Nitamtukuza Bwana nyakati zote, 2 sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote. 1

2Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, 2 walioonewa watasikia na wafurahi. 1

3Mtukuzeni Bwana pamoja nami, 2 naam, na tulitukuze jina lake pamoja. 1

4Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, 2 akaniokoa kwenye hofu zangu zote. 1

5Wale wamtazamao hutiwa nuru, 2 nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. 1

6Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, 2 akamwokoa katika taabu zake zote. 1

7Malaika wa Bwana hufanya kituo 2 akiwazunguka wale wamchao, 2 naye huwaokoa. 1

8Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, 2 heri mtu yule anayemkimbilia. 1

9Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, 2 kwa maana wale wamchao 2 hawapungukiwi na chochote. 1

10Wana simba wenye nguvu 2 hutindikiwa na kuona njaa, 1 bali wale wamtafutao Bwana 2 hawatakosa kitu chochote kilicho chema. 1

11Njooni, watoto wangu, mnisikilize, 2 nitawafundisha kumcha Bwana. 1

12Yeyote kati yenu anayependa uzima 2 na kutamani kuziona siku nyingi njema, 1

13basi auzuie ulimi wake na mabaya, 2 na midomo yake kutokana na kusema uongo. 1

14Aache uovu, atende mema, 2 aitafute amani na kuifuatilia. 1

15Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, 2 na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao. 1

16Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, 2 ili kufuta kumbukumbu lao duniani. 1

17Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, 2 huwaokoa katika taabu zao zote. 1

18Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, 2 na huwaokoa waliopondeka roho. 1

19Mwenye haki ana mateso mengi, 2 lakini Bwana humwokoa nayo yote, 1

20huhifadhi mifupa yake yote, 2 hata mmoja hautavunjika. 1

21Ubaya utamuua mtu mwovu, 2 nao adui za mwenye haki watahukumiwa. 1

22Bwana huwakomboa watumishi wake, 2 yeyote anayemkimbilia yeye 2 hatahukumiwa kamwe.

← Psalms 33Read In The App, Free →Psalms 35 →

Study Psalms 34

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150