Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 33

1Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki; 2 kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. 1

2Msifuni Bwana kwa kinubi, 2 mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. 1

3Mwimbieni wimbo mpya; 2 pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe. 1

4Maana neno la Bwana ni haki na kweli, 2 ni mwaminifu kwa yote atendayo. 1

5Bwana hupenda uadilifu na haki; 2 dunia imejaa upendo wake usiokoma. 1

6Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, 2 jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake. 1

7Ameyakusanya maji ya bahari 2 kama kwenye chungu; 1 vilindi vya bahari 2 ameviweka katika ghala. 1

8Dunia yote na imwogope Bwana, 2 watu wote wa dunia wamche. 1

9Kwa maana Mungu alisema, na ikawa, 2 aliamuru na ikasimama imara. 1

10Bwana huzuia mipango ya mataifa, 2 hupinga makusudi ya mataifa. 1

11Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele, 2 makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote. 1

12Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, 2 watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake. 1

13Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini 2 na kuwaona wanadamu wote; 1

14kutoka maskani mwake huwaangalia 2 wote wakaao duniani: 1

15yeye ambaye huumba mioyo yao wote, 2 ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda. 1

16Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake; 2 hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake. 1

17Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu, 2 licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa. 1

18Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, 2 kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo, 1

19ili awaokoe na mauti, 2 na kuwahifadhi wakati wa njaa. 1

20Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, 2 yeye ni msaada wetu na ngao yetu. 1

21Mioyo yetu humshangilia, 2 kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. 1

22Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, 2 tunapoliweka tumaini letu kwako.

← Psalms 32Read In The App, Free →Psalms 34 →

Study Psalms 33

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150