Psalms 50
1Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana, 2 asema na kuiita dunia, 1 tangu mawio ya jua 2 hadi mahali pake liendapo kutua. 1
2Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, 2 Mungu anaangaza. 1
3Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, 2 moto uteketezao unamtangulia, 2 akiwa amezungukwa na tufani kali. 1
4Anaziita mbingu zilizo juu, 2 na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: 1
5“Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, 2 waliofanya agano nami kwa dhabihu.” 1
6Nazo mbingu zinatangaza haki yake, 2 kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu. 1
7“Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, 2 ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: 2 Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu. 1
8Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, 2 au sadaka zako za kuteketezwa, 2 ambazo daima ziko mbele zangu. 1
9Sina haja ya fahali wa banda lako, 2 au mbuzi wa zizi lako. 1
10Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, 2 na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. 1
11Ninamjua kila ndege mlimani, 2 nao viumbe wa kondeni ni wangu. 1
12Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi, 2 kwa maana ulimwengu ni wangu, 2 pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. 1
13Je, mimi hula nyama ya mafahali 2 au kunywa damu ya mbuzi? 1
14Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, 2 timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, 1
15na uniite siku ya taabu; 2 nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
16Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: 1 “Una haki gani kunena sheria zangu 2 au kuchukua agano langu midomoni mwako? 1
17Unachukia mafundisho yangu 2 na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 1
18Unapomwona mwizi, unaungana naye, 2 unapiga kura yako pamoja na wazinzi. 1
19Unakitumia kinywa chako kwa mabaya 2 na kuuongoza ulimi wako kwa hila. 1
20Wanena daima dhidi ya ndugu yako 2 na kumsingizia mwana wa mama yako. 1
21Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, 2 ukafikiri Mimi nami ni kama wewe. 1 Lakini nitakukemea 2 na kuweka mashtaka mbele yako. 1
22“Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu, 2 ama sivyo nitawararua vipande vipande, 2 wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa: 1
23Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, 2 naye aiandaa njia yake 2 ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.”